Rais wa Kenya afanya mabadiliko ya Baraza lake la Mawaziri
5 Oktoba 2023Matangazo
Waziri wa mambo ya nje Alfred Mutua amehamishwa katika wizara ya utalii na wanyamapori huku waziri wa biashara Moses Kuria akihamishwa kwenye wizara ya utumishi wa umma. Wizara ya mambo ya nje itakuwa chini ya mamlaka ya waziri mkuu Musalia Mudavadi.
Rais Ruto amesema mabadiliko hayo yalikuwa muhimu ili kuboresha utendaji kazi kama ilivyoainishwa katika ilani ya utawala.
Ruto aliyeingia madarakani Agosti mwaka 2022, amekuwa akikabiliwa na msururu wa maandamano ya nchi nzima ambapo Wakenya wamekuwa wakilalamika kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha na ongezeko la ushuru.