1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Sierra Leone aongoza matokeo ya uchaguzi

Sylvia Mwehozi
27 Juni 2023

Rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone anaongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais baada ya asilimia 60 ya kura kuhesabiwa.

https://p.dw.com/p/4T6eR
Sierra Leone | Wahlen | Julius Maada Bio
Picha: JOHN WESSELS/AFP/Getty Images

Bio, ambaye anawania kiti cha urais kwa muhula wa pili, anapambana na wagombea wengine 12 akiwemo mpinzani wake mkuu, Samura Kamara, aliyeshindwa katika uchaguzi uliopita wa 2018. 

Tume ya uchaguzi imesema matokeo yasiyo rasmi yanaonyesha kwamba Bio amejizolea kura zaidi ya milioni moja akifuatiwa na Kamara aliye na kura chini ya laki 800,000.

Soma zaidi: Wananchi Sierra Leone wasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu

Raia wa Sierra Leone wanapiga kura kumchagua rais, wabunge na madiwani.


Matokeo hayo tayari yanapingwa na chama cha upinzani cha All People's Congress APC, ambacho kimesema uchaguzi ulikuwa na hitilafu hasa za ujumuishaji, uwazi na uwajibikaji wa tume ya uchaguzi.

Waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya wamesema kukoskana kwa uwazi na mawasiliano kutoka kwa Tume ya Uchaguzi kumechangia mchakato wa uchaguzi kutoaminika.