Rais wa Somalia anaongoza kikao cha mkutano wa kilele
14 Mei 2024Matangazo
Viongozi wa majimbo ya kusini magharibi ya Jubaland na Galmudug wameshawasili mjini Mogadishu kushiriki mkutano huo wa kilele wa kitaifa ambao awali ulikuwa umepangwa kuandaliwa Aprili 20 lakini ukaakhirishwa kufuatia mivutano ya kisiasa iliyozuka kuhusu mageuzi ya sheria za nchi. Bado haijafahamika ikiwa viongozi wa majimbo ya Hirshabelle na Puntland watashiriki. Majimbo hayo yanatajwa kusitisha ushirikiano na serikali kuu kupinga mageuzi ya katiba. Mkutano huo pia utajadili kuhusu mvutano wa hivi karibuni kati ya Somalia na jirani yake Ethiopia. Kadhalika mkutano huo umeandaliwa katika wakati ambapo rais Mohamud kesho anaadhimisha miaka miwili tangu alipoingia madarakani.