Rais wa Zimbabwe akosolewa na Upinzani
4 Agosti 2023Chamisa amesema Mnangagwa anatumia taasisi kama vile polisi na mahakama kuwachukulia hatua kali watu muhimu, kupiga marufuku mikutano ya upinzani na kuzuia baadhi ya watu kugombea.
Soma pia: Sheria tata ya "uzalendo" yaanza kutumika Zimbabwe
Ameonya pia kwamba ushahidi wowote wa uchakachuaji matokeo utakaobainika kuendeshwa na chama tawala cha Mnangagwa katika uchaguzi wa mwezi huu, unaweza kusababisha maafa makubwa kwa taifa hilo linalokabiliwa na matatizo ya kiuchumi na ambalo tayari lipo chini ya vikwazo vya Marekani na Umoja wa Ulaya kutokana na rekodi yake ya haki za binadamu.
Soma pia: Zimbabwe yaomba msaada wa fedha kutoka Afrika Kusini
Chamisa atachuana na Mnangagwa wa chama tawala cha Zanu-PF kilicho madarakani kwa miaka 43, katika uchaguzi wa rais utakaofanyika Agosti 23 mwaka huu.