1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Rais Xi apongeza uhusiano wa China na Urusi

20 Machi 2023

Rais wa China, Xi Jinping amepongeza uhusiano wa karibu na Urusi. Pongezi hizo amezitoa leo katika Ikulu ya Urusi, Kremlin alipokutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake Rais Vladmir Putin.

https://p.dw.com/p/4Owi6
China Peking | Wladimir Putin und Xi Jinping Februar 2022
Picha: Alexei Druzhinin/AP/picture alliance

Xi amemshukuru Putin kwa kile alichokiita uungaji wake mkono kwa China. Ziara ya Xi inapeleka ujumbe mzito kwa viongozi wa nchi za Magharibi ambao ni washirika wa Ukraine kwamba juhudi zao za kuitenga Urusi zimekwama.

Hiyo ni ziara ya kwanza ya Xi tangu Putin alipoivamia Ukraine, Februari mwaka uliopita. Wakati huo huo, Ukraine imesema inaifuatilia kwa karibu ziara ya Xi, na imemtaka kiongozi huyo wa China kutumia ushawishi wake kuishinikiza Urusi kukomesha vita.

Soma pia: Rais wa China Xi aelekea Urusi katika ziara ya 'amani'

Uingereza pia imesema Xi anapaswa kumshinikiza Rais Putin kukomesha vita na ukatili nchini Ukraine.