1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia yaandaa mazungumzo ya kumaliza vita vya Ukraine

5 Agosti 2023

Saudi Arabia ni mwenyeji wa mazungumzo juu ya vita vya Ukraine licha ya matumaini ya kufanikiwa kuwa finyu. Mazungumzo hayo yanahudhuriwa na washauri wa usalama wa kitaifa na maafisa wengine kutoka nchi zipatazo 30.

https://p.dw.com/p/4Uo7x
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: president.gov.ua

Mkutano huo unaofanyika leo mjini Jeddah, unashiria utayarifu wa Saudi Arabia wa kutoa mchango wake ili kuleta suluhisho la amani ya kudumu. Urusi haitahudhuria mkutano huo. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameunga mkono kufanyika mkutano huo unaohudhuriwa na wajumbe kutoka nchi mbalimbali ikiwa pamoja na nchi zinazoendelea ambazo zimeathirika na kupanda kwa bei za vyakula kutokana na vita.

Soma zaidi: China kushiriki mazungumzo ya Jeddah kuhusu mpango wa amani wa Ukraine

Zelensky amesema mazungumzo ya mjini Jeddah ni muhimu kwa sababu masuala ya chakula, usalama na hatma ya mamilioni ya watu duniani yanategemea juhudi zitakavyofanyika ili kuutekeleza mpango wa amani. China ambayo imekataa kuilaani Urusi kwa kuivamia Ukraine pia inawakilishwa kwenye mkutano huo wa mjini Jeddah.