Saudi Arabia yaisadia Yemen dola milioni 250
12 Februari 2024Pesa hizo zinatolewa baada ya malipo ya awali ya kiasi kama hicho yaliyotangazwa mwezi Agosti, wakati serikali ya Riyadh ilipojitolea kutoa jumla ya dola bilioni 1.2 ili kupunguza nakisi ya bajeti ya serikali na kulipa mishahara kwa watumishi wa umma. Balozi wa Saudia nchini Yemen, Mohammed al Jaber amesema awamu ya pili ruzuku ya kusaidia kushughulikia nakisi ya bajeti ya serikali ya Yemen iliingizwa katika Benki Kuu ya Yemen huko Aden, kiasi cha dola milioni 250 kusaidia mishahara na malipo matumizi mengine. Serikali ya Yemen ilihamishiwa Aden, mji wa bandari wa pwani ya kusini, baada ya waasi wa Huthi wanaoungwa mkono na Iran kuuteka mji mkuu wa Sanaa mwaka 2014. Mwaka wa 2015 Saudi Arabia ilianzisha muungano wa kimataifa wa kijeshi ulionuia kuwatimua Wahuthi.