Semenya ashinda rufaa kushiriki michezo ya dunia
11 Julai 2023Mahakama ya Haki za Binaadamu ya Ulaya imeamua kwamba mwanariadha huyo alibaguliwa.
Uamuzi huo huenda ukailazimisha Mahakama ya Juu zaidi ya michezo kutathmini upya sheria zake zilizomlazimisha Semenya na wanariadha wengine wa kike kupunguza viwango vya homoni za Testerone ili kuruhusiwa kushiriki katika Mashindano ya Olimpiki.
Soma zaidi: Mahakama ya CAS yaanza kusikiliza kesi ya Semenya
Semenya apeperusha Bendera ya Afrika Kusini Olimpik
Mahakama hiyo yenye makao makuu yake mjini Strasbourg, Ufaransa, imeeleza kuwa mwanariadha huyo wa Afrika Kusini alinyimwa haki baada ya Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo kupinga rufaa dhidi ya sheria za kumzuia kushiriki katika mashindano ya dunia.
Hata hivyo, haikubainika mara moja iwapo uamuzi huo utalazimisha kuondololewa kwa sheria hizo na kumruhusu Semenya mwenye umri wa miaka 32 kushiriki katika mashindano ya Olimpiki mwaka ujao mjini Paris.