Senegal: Rais Sall asema ataachia madaraka muda wake ukifika
23 Februari 2024Matangazo
Sall anakabiliwa na shinikizo la kupanga tarehe ya kupiga kura baada ya kuucheleweshw uchaguzi uliotarajiwa kufanyika Februari 25 hali iliyosababisha mgogoro wa wiki kadhaa.
Huku kukiwa na mvutano wa kijamii na kisiasa, Rais wa Senegal amesema hatotangaza tarehe mpya ya uchaguzi mpaka baada ya mazungumzo ya kisiasa yanayotarajiwa kuanza wiki ijayo ambapo Sall atafanya majadiliano Jumatatu na Jumanne na wagombeaji urais na wahusika wengine wa kisiasa na kijamii nchini humo.
Katika hatua inayoonekana ya kutuliza maoni ya umma, rais Sall amesema anafikiria kuwaachilia huru viongozi wa upinzani Ousmane Sonko na Bassirou Diomaye Faye walio kizuizini.