SiasaSerbia
Serbia, Kosovo washindwa kurejesha uhusiano wa kidiplomasia
19 Machi 2023Matangazo
Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic walikutana kwa mazungumzo ya saa 12 kwenye mwambao wa Ziwa Ohrid, huko Macedonia Kaskazini, chini ya usaidizi wa mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell. Umoja wa Ulaya hata hivyo umepongeza maendeleo yaliyofikiwa.
Soma pia: Mkutano wa Serbia na Kosovo umemalizika bila maafikiano
Katika miezi ya hivi karibuni, mataifa ya Magharibi yamekuwa yakiongeza shinikizo kwa Belgrade na Pristina ili kutatua mzozo wao na kuzuia uwezekano wa kuzuka kwa mvutano katika eneo tete la Balkan wakati uvamizi wa Urusi ukiendelea huko Ukraine.
Serbia inakataa kuutambua uhuru wa jimbo lake la zamani la Kovoso uliotangazwa mwaka 2008.