Sudan yalaani vikwazo vya Marekani dhidi ya Burhan
17 Januari 2025Katika taarifa yake, wizara hiyo imesema vikwazo hivyo vinaleta mkanganyiko baada ya miezi 21 ya vita kati ya jeshi na vikosi vya RSF, huku ikisisitiza kuwa Burhan anawatetea watu wa Sudan dhidi ya kile ilichotaja kuwa njama ya mauaji ya kimbari.
Siku ya Alhamisi, wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza vikwazo dhidi ya Burhan, ikilishutumu jeshi kwa kushambulia shule, masoko na hospitali na kutumia chakula kama silaha ya vita.
Soma pia: UN yaonya kuhusu mashambulizi ya kulipiza kisasi Sudan
Haya yanajiri wiki moja baada ya Marekani kumuwekea pia vikwazo kiongozi wa RSF Mohamed Hamdan Daglo, ikilishutumu kundi lake kwa kufanya mauaji ya halaiki. Tangu kuanza kwa mzozo huo Aprili mwaka 2023, pande zote mbili zimekuwa zikishutumiwa kwa kuwalenga raia na kushambulia kwa makombora maeneo ya makazi.