1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Shambulio la Israel laua watu watano katika ukanda wa Gaza

8 Januari 2025

Madaktari wa Palestina wamesema mashambulizi ya anga ya Israel yamesababisha vifo vya watu watano katika Ukanda wa Gaza, wakiwemo watoto wawili wachanga na mwanamke.

https://p.dw.com/p/4ow9C
Ukanda wa Gaza | Uharibifu baada ya shambulizi la Israel
Sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza imesalia magofu kufuatia vita vya Israel na HamasPicha: BASHAR TALEB/AFP/Getty Images

Madaktari wa Palestina wamesema mashambulizi ya anga ya Israel yamesababisha vifo vya watu watano  katika Ukanda wa Gaza, wakiwemo watoto wawili wachanga na mwanamke.

Shambulio moja lilipiga nyumba moja katikati mwa mji wa Deir al-Balah na kusababisha vifo vya wanaume wawili na mwanamke, kwa mujibu wa Hospitali ya Al-Aqsa, ambayo imewapokea wahanga wa shambulio hilo.

Soma pia: Watoto 7 wamekufa kwa baridi kali Gaza huku makumi wakiuawa

Shambulio lingine lilipiga nyumba moja katika eneo la Sheikh Radwan kulingana na ripoti ya wizara ya afya ya Gaza.

Jeshi la Israel limesema limefanya mashambulizi hayo kuwalenga wapiganaji wa Hamas ambao wanajificha katika maeneo hayo.

Vita hivyo vilianza wakati wanamgambo wa Hamas walipovamia kusini mwa Israel mnamo Oktoba 7, 2023, na kuua watu wapatao 1,200 na kuwateka nyara watu 250. Mateka 100 bado wako wanashikiliwa na kundi hilo.