1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Shambulio la Urusi kwenye mji wa Odessa laua mtu 1

15 Novemba 2024

Mtu mmoja ameuawa na wengine 10 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la anga la Urusi kwenye majengo ya makazi na mitambo ya nishati kwenye mji wa bandari wa Odesa.

https://p.dw.com/p/4n13H
Mji wa Odessa.
Athari za vita nchini Ukraine.Picha: Nina Liashonok/REUTERS

Gavana wa mkoa wa Odessa Oleh Kiper ameeleza kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Telegram kuwa mashambulizi hayo yalisababisha uharibifu mkubwa huku karibu magari 30 yakiteketea moto.

Naye Meya wa Odesa Hennadiy Trukhanov amesema shambulio hilo limewaacha zaidi ya watu 40,000 bila ya kuwa na uwezo wa kupasha joto majumba yao, huku miundombinu ya hospitali moja inayohudumia wanawake wajawazito ya jiji hilo ikiwa pia imeharibiwa.