Shambulizi la droni laelekezwa nyumbani kwa Netanyahu
19 Oktoba 2024Ving'ora vimelia leo asubuhi nchini humo kuonya mashambulizi kutoka Lebanon.
Katika taarifa yake, msemaji wa Netanyahu amesema waziri huyo mkuu na mkewe hawakuwepo nyumbani wakati wa mashambulizi hayo. Bado haijaeleweka wazi ikiwa droni hiyo ilirushwa kutokea upande gani miongoni mwa pande zinazopambana na Israel.
Hezbollah yadai kurusha kombora kuelekea mji wa Haifa nchini Israel
Kwa upande wake, kundi la Hezbollah nchini Lebanon linasema limerusha makombora yake kuelekea mji wa kaskazini mwa Israel wa Haifa mapema leo.
Soma pia:Israel yaendelea kuishambulia Gaza baada kifo cha Sinwar
Mzozo pia unaendelea kati ya Israeli na Hamas katika ukanda wa Gaza, huku pande zote mbili zikionesha hakuna matumaini ya kumalizika kwa vita hata baada ya kifo cha kiongozi wa Hamas, Yahya Sinwar wiki hii.
Hapo jana, kiongozi mkuu wa Iran, Ayatullah Ali Khamenei, alisema kifo cha Sinwar kilikuwa pigo kubwa lakini mapambano bado yanaendelea.