SiasaMamlaka ya Palestina
Mamlaka ya Palestina yatangaza baraza jipya la mawaziri
28 Machi 2024Matangazo
Mawaziri wote aliowataja hawana umaarufu mkubwa. Karibu watano kati ya mawaziri 23 wanaoingia serikalini wanatokea Gaza ingawa haijajulikana iwapo bado wapo katika eneo hilo.
Tafiti za maoni za miaka ya hivi karibuni zimeonesha kwamba Wapalestina walio wengi wanamtaka Abbas mwenye umri wa miaka 88 aachie ngazi.
Mamlaka ya Palestina inasimamia sehemu ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Waisraeli na haina mamlaka Gaza baada ya majeshi yake kufukuzwa baada ya kundi la Hamas kuchukua madaraka mwaka 2007.
Wapalestina wachache ndio wanaoiunga mkono mamlaka hiyona hasa kwa sababu ya kutofanyika uchaguzi katika kipindi cha miaka 18.