Starmer aitisha mkutano wa dharura kujadili ghasia
5 Agosti 2024Katika vurugu hizo, majengo na magari yameteketezwa kwa moto huku hoteli wanamolala wageni wanaotafuta hifadhi nchini Uingereza zikishambuliwa.
Wiki iliyopita, machafuko yalizuka katika sehemu mbalimbali nchini humo baada ya wasichana watatu kuuawa katika shambulio la kisu mjini Southport, kaskazini magharibi mwa Uingereza huku watu 420 wakikamatwa hadi sasa.
Soma zaidi: Waziri Mkuu Starmer aapa kuwawajibisha walioshiriki ghasia
Machafuko hayo yamechochewa na taarifa za uongo zilizosambazwa mitandaoni na makundi yanayopinga wahamiaji na Waislamu kwamba waliohusika na mauaji ya wasichana hao watatu ni Muislamu mwenye itikadi kali za kidini aliyewasili Uingereza hivi karibuni.
Polisi, hata hivyo, wamesema mshukiwa wa mauaji hayo ni mzaliwa wa Uingereza na hawalichukulii tukio hilo kama la kigaidi.