Sudan Kusini kuanza tena kuuza mafuta ghafi nje ya nchi
25 Oktoba 2024Matangazo
Afisa mmoja wa serikali ya Sudan Kusini ameliambia shirika la Habari la Reuters kwamba kazi hiyo ya kupampu mafuta itaanza baada ya kumalizika ukarabati wa bomba kuu lililopasuka, wakati wa mapigano nchini Sudan kati ya jeshi la Sudan SAF na Kikosi cha wanamgambo waRSF yaliyoanza mwezi Aprili mwaka jana. Mafuta yanayosafirishwa kupitia bomba la mafuta nchini Sudan ni chanzo muhimu cha mapato kwa Sudan Kusini, yanayowakilisha asilimia 90 ya mapato yake ya fedha za kigeni. Sudan pia inapata malipo kama ada ya usafirishaji wa mafuta ya Sudan Kusini kupitia kwenye bandari yake. Sudan Kusini imekuwa ikisafirisha kati ya mapipa laki moja hadi laki moja na nusu ya mafuta ghafi kwa siku hadi nchini Sudan kwa ajili ya kuuza nje.