1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAlgeria

Sweden yalaani uvamizi wa ubalozi wake, Baghdad

20 Julai 2023

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden imesema inawasiliana na maafisa wa ngazi ya juu nchini Iraq ili kuwaelezea masikitiko yake kuhusiana na tukio la usiku wa kuamkia leo, Jumatano.

https://p.dw.com/p/4UA9S
Busunglück in Algerien
Picha: Algerian Civil Protection/REUTERS

Inaarifiwa kuwa waandamanaji wameuvamia na kuuchoma moto Ubalozi wa Sweden mjini Baghdad.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Tobias Billström amesema tukio hilo halikubaliki na ni wazi kwamba mamlaka za Iraq zimeshindwa katika wajibu wao wa kuulinda ubalozi huo na wafanyakazi wake.

Haya yanajiri baada ya tukio la hivi karibuni la uchomaji wa kitabu kitakatifu kwa Waislamu, Qur'an, kufanyika kwenye mji mkuu wa Sweden, Stockholm.

Tukio hilo lilizusha ghadhabu miongoni mwa Waislamu duniani kote.