1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chile: Waliokufa katika moto wa msituni wapindukia 100

5 Februari 2024

Takriban watu 112 wamepoteza maisha kufuatia moto mkali wa msituni katika mkoa wa Valparaiso nchini Chile. Rais wa nchi hiyo Gabriel Boric ametangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4c2on
Chile I moto wa msituni
Maafisa wakipambana kuuzima moto huko ChilePicha: Javier Torres/AFP

Takriban watu 112 wamepoteza maisha kufuatia moto mkali wa msituni katika mkoa wa Valparaiso nchini Chile. Rais wa nchi hiyo Gabriel Boric ametangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Jumatatu kwa aajili ya kuwaenzi waliopoteza maisha katika janga hilo.

Akizungumza jana wakati alipokutana na waathirika kwenye eneo lilikotokea janga hilo,rais Boric alisema,moto huo ni janga kubwa kuwahi kuikumba Chile tangu mwaka 2010 lilipotekea tetemeko la ardhi,ambapo watu 520 waliuwawa.Waziri wa mambo ya ndani nchini humo,Carolina Toha amesema ,idadi ya waliokufa na majeruhi kutokana na moto ya msituni inatarajiwa kuongezeka.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW