1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaChile

Watu 99 wafariki kufuatia moto wa nyika huko Chile

5 Februari 2024

Idadi ya vifo kutokana na moto mkali wa mwituni nchini Chile imeongezeka hadi kufikia watu 99 huku wengine karibu 1,600 wakiachwa bila makazi.

https://p.dw.com/p/4c2OU
Chile I Moto wa nyika
Maafisa wa zima moto wakijaribu kukabiliana na moto huo wa nyika nchini ChilePicha: Javier Torres/AFP

Vikosi vya uokozi vinaendelea kupambana na moto huo ambao umejikita katika maeneo ya watalii ya Viña del Mar na Valparaiso, ambapo umeharibu mamia ya hekta za misitu. Katika eneo la Valparaiso, takriban nyumba 3000 zimeteketea kwa moto. Karibu watu 200 hadi sasa haijulikani walipo.

Alipotembelea mji wa Quilpé ambao umeathirika pia na moto huo,  Rais wa Chile Gabriel Boric  ametangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa kuanzia Jumatatu huku akiamuru kutumia rasilimali zote muhimu ili kukabiliana na moto huo.