Tanzania yazindua ramani ya kidigitali ya mashirika binafsi
28 Septemba 2023Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na makundi Maalum nchini Tanzania Dkt. Dorothy Gwajima, amesema wakati akizindua mfumo huo, kwamba serikali itaendelea kudhibiti utendaji wa mashirika yasio ya kiserikali ili kubaini yale ambayo yanakwenda kinyume na sheria na kanuni za nchi na kuyachukulia hatua za kisheria.
Mbali na hilo, Waziri Gwajima amesema kuwa mfumo huo utayasaidia mashirika hayo katika utendaji wa shughuli zake mbali mbali na kurahisisha mawasiliano kati ya pande zote mbili na kuongeza kuwa.
Mfumo huo unatajwa kuwa na uwezo wa kutambua mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanafanya nini na kusaidia kujua fursa mbalimbali zinazotolewa na mashirika hayo. Bi. Vickness Mayao ni Msajili wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali nchini Tanzania.
Hisia tofauti za wadau
Hata hivyo kuzinduliwa kwa mfumo huo wa kidijitali wenye lengo ya kuyamulika na kusaidia utendaji kazi kwa mashirika hayo umepokelewa kwa hisia tofauti kutoka kwa wadau wa asasi za kiraia. Bwana Odero Charles Odero anafanya kazi na Shirika la kutetea haki za binadamu pamoja na haki za kiraia lililoko Arusha kaskazini mwa Tanzania, anasema.
Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yamekuwa na mchango mkubwa nchini Tanzania katika kusaidia kutekeleza program mbalimbali ikiwemo afya pamoja na elimu na hadi kufikia Septemba 22 mwaka huu zaidi ya Mashirika 1900 yamesajiliwa na kati ya Mashirika hayo ya Kimataifa ni 588.
Hata hivyo baadhi ya mashirika hayo yamelaumiwa kwa kutumia udhaifu katika mfumo wa usimamizi na kufanya mambo yanayokwenda kinyume na sheria za nchi na utamaduni wa Kiafrika, ikiwemo kukuza vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.