1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAmerika ya Kaskazini

Trump kurejea tena mahakamani siku ya Jumanne

16 Aprili 2024

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kurejea katika mahakama ya mjini New York leo, wakati jaji akitafuta jopo la majaji ambao wataamua iwapo ana hatia ya mashtaka ya jinai.

https://p.dw.com/p/4eqTw
New York, Marekani |  Donald Trump akiwa katika mahakama ya Manhattan.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa mahakamani kufuatilia kesi dhidi yake.Picha: Jabin Botsford/REUTERS

Rais huyo wa zamani wa Marekani ambae anawania kurejea Ikulu, anakabiliwa na hatia ya mashtaka ya jinai, kufuatia madai kwamba alighushi rekodi za biashara ili kuficha kashfa ya ngono wakati wa kampeni mwaka 2016.

Siku ya kwanza ya kesi hiyo ya kihistoria dhidi ya Trump huko Manhattan ilimalizika bila ya jaji yeyote kuchaguliwa kuwa kwenye jopo la majaji 12 na wengine sita wa mbadala.

Majaji kadhaa walikataliwa baada ya kusema hawakuwaamini wanaweza kutenda haki.

Soma pia:Kesi ya kihistoria dhidi ya Trump yaanza New York

Hiyo ndiyo kesi ya kwanza kati ya nne za jinai dhidi ya Trump kusikizwa na huenda ndiyo itakuwa pekee ambayo uamuzi utafikiwa kabla ya uchaguzi wa mwezi Novemba utakaoamua ikiwa ataweza kuchaguliwa tena.