1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump, Netanyahu wakutana na kuondoa uvumi wa kuwepo mvutano

27 Julai 2024

Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump amekutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Florida na kutumia fursa hiyo kumshambulia mpinzani wake Kamala Harris.

https://p.dw.com/p/4ioSm
Mar-a-Lago | Trump na Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mkewe Sara (kulia) wakikaribishwa na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump Mar-a-Lago mjini Florida.Picha: Israeli Government Press Office/AFP

Mkutano kati ya Trump na Netanyahu umeondoa kabisa uvumi juu ya kuwepo kwa mvutano kati yao.

Mkutano huo pia ulikuwa wa kwanza wa ana kwa ana kati ya wawili hao tangu Trump alipoondoka Ikulu ya White House zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Soma pia: Biden kukutana na Netanyahu 

Netanyahu yuko ziarani nchini Marekani na tayari amefanya mkutano na Rais Joe Biden na makamu wake Kamala Harris baada ya kulihubutia bunge la Congress.

Biden na Harris wamemtolea mwito waziri mkuu huyo wa Israel kufanya kila awezalo kulinda raia katika vita vinavyoendelea ukanda wa Gaza.