SiasaVenezuela
Uchaguzi Mkuu unaosubiriwa Venezuela kufanyika mwezi Juni
6 Machi 2024Matangazo
Tangazo la tarehe hiyo ya uchaguzi limetolewa na rais wa tume ya taifa ya uchaguzi Elvis Amoroso. Uamuzi huo wa kufanya uchaguzi mwezi Juni umekwenda sambamba na matakwa ya upinzani ulioshinikiza kuwepo muda wa kutosha kuboresha daftari la wapigakura na vyama kujitayarisha kwa kampeni.
Rais Nicolas Maduro anatazamiwa kuwania muhula mwingine madarakani. Hata hivyo mpinzani wake mkuu Maria Corina Machado bado amepigwa marufuku kushiriki uchaguzi huo.
Mnamo mwezi Januari Mahakama ya Juu ya Venezuela ilipilia msumari uamuzi wa kumzuia Machado kushiriki uchaguzi kwa miaka 15 baada ya kutiwa hatiani kwa kushiriki njama ya kula rushwa.