Uchaguzi wa mapema Uhispania kizungumkuti viti vingi bungeni
24 Julai 2023Baada ya kuhesabiwa kura zote, chama cha Alberto Nunez Feijoo cha Popular Party - PP na cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Vox --kinachoweza kuwa mshirika wake -- vilipata jumla ya viti 169, na kushindwa kufikia idadi ya wingiwa viti 176 inayohitajika ili kuunda serikali.
Soma pia:Wahispania wajitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Jumapili
Wasoshalisti wa Sanchez na chama cha itikadi kali za mrengo wa kushoto Sumar walipata viti 153.
Sasa Wasoshalisti hao kile cha Sumar watahitaji uungwaji mkono wa vyama kadhaa vya kikanda kama vile cha siasa za mrengo wa kushoto kinachopigania kujitenga jimbo la Catalan cha ERC.
Kama watashindwa, Uhispania ambayo imefanya uchaguzi mkuu mara nne kati ya 2015 na 2019 huenda kwa mara nyingine ikajikuta katika mkwamo na kulazimika kuitisha uchaguzi mpya.