Uchunguzi wa ajali ya ndege ya Yemenia waanzishwa Ufaransa
9 Mei 2022Uchunguzi wa mahakama unafanyika wakati wawakilishi wa shirika hilo la ndege wakikosa kujiwasilisha katika mahakama hiyo wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini Yemen.
Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa kwa kipindi cha wiki nne na iwapo watakutwa na kosa watatozwa faini ya euro 225,000 kwa kusababisha mauaji na majeraha kwa binadamu.
Tarehe 29 ya Mwezi Juni mwaka 2009 ndege hiyo aina ya Yemenia chapa 626 ilikuwa inakaribia jiji kuu la visiwa vya la Comoro, Moroni eneo jirani na taifa la Msumbiji na Madagascar kabla ya kuanguka katika Bahari ya Hindi.
Abiria wote waliokuwa wameabiri ndege hiyo walifariki kwenye ajali hiyo isipokuwa Bahia Bakari, wakati huo akiwa mtoto mwenye umri wa miaka 12.
Kati ya abiria 142 waliokuwa kwenye chombo hicho walikuwa wahudumu 11 wa ndege hiyo na raia 66 wa Ufaransa waliokuwa wahehamishwa katika uwanja wa ndege wa Sanaa wakati huo.
Soma pia →Aliyenusurika katika ajali ya ndege ya Yemenia awasili Ufaransa
Kumbukumbu ya ajili
Bakari Bahia katika kitabu chake alichokiandika anaeleza yaliomkumba baada ya ajali hiyo kabla ya kuokolewa siku ifuatayo baada ya kukaa baharini kwa saa kumi na moja.
Ufaransa ilituhumu mamlaka nchini Comoro kwa kuchelewesha uchunguzi wa kubaini chanzo cha ajali hiyo familia za waathiriwa nazo zikiituhumu Yemen kwa kupanga kuhujumu uchunguzi dhidi ya shirika lake la ndege.
Kesi hiyo inaanza kusikilizwa baada ya miaka 13 ya kusubiri haki japokuwa wachunguzi na wataalam wa mambo ya usafiri wa angani walibaini kuwa ndege hiyo haikuwa na changamoto zozote za kiufundi ila wahudumu wake walikosea wakati ndege hiyo ilipokuwa inatarajia kutua jijini Moroni kabla ya chombo hicho hakijapoteza mwelekeo.
Soma pia →Ajali ya ndege.
Karibia watu 560 wamejumuishwa katika orodha ya wanaolalamika, wengi wao wakitokea mjini Marseille kusini mwa Ufaransa nyumbani kwa watu wengi walioathirika na ajali hiyo ya mwaka wa 2009.