Ufaransa yaahidi kuunga mkono mpango wa ushindi wa Ukraine
19 Oktoba 2024Katika mkutano wa pamoja wa waandishi habari akiwa na mwenzake wa Ukraine, Andrii Sybiha, hivi leo, waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, alisema kwamba angelishirikiana na maafisa wa Ukraine kupata uungaji mkono wa mataifa mengine kwa mpango huo wa amani ya kudumu.
Barrot ameongeza kuwa ushindi wa Urusi utakuwa kile alichokiita, kuhalalisha sheria ya porini ya mwenye nguvu ndiye mwenye haki na kuuingiza mfumo wa kimataifa kwenye machafuko makubwa.
Ufaransa yaahidi msaada wa ndege za kijeshi kwa Ukraine
Waziri huyo wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa alisema nchi yake itaikabidhi Ukraine sehemu ya mwanzo ya msaada wa ndege za kijeshi ndani ya kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka 2025.
Ufaransa pia itatowa mafunzo kwa marubani ili waweze kuziendesha wenyewe na mafundi wa ndege ili waweze kuzitengeneza wenyewe.