1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Urusi yaongeza shinikizo kwa kushambulia zaidi Donestk

16 Oktoba 2024

Mamlaka za kijeshi nchini Ukraine zimesema wanajeshi wa Urusi wanazidisha shinikizo kwenye kijiji cha Kurakhivka katika mkoa wa mashariki wa Donetsk ambako kumeripotiwa mashambulizi yapatayo 40 kwa siku moja.

https://p.dw.com/p/4lrSN
Vikosi vya Urusi vyaongeza shinikizo kwa kushambulia zaidi Donestk
Vikosi vya Urusi vyaongeza shinikizo kwa kushambulia zaidi DonestkPicha: ROMAN PILIPEY/AFP

Hata hivyo jeshi la Kiev limesema limefanikiwa kuwazuia askari wa Urusi kusonga mbele huku wanablogu wa Ukraine wakiripoti kuwa vikosi vya Moscow vimechukua udhibiti wa kijiji cha Ostrivske, kusini mwa Kurakhivka.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa Jumatano (16.10.2024) kuwasilisha bungeni mpango wake unaotajwa kuwa na mikakati ya kuvimaliza vita hivyo.  

Hivi karibuni Zelensky alifanya ziara kwa washirika wake wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na Marekani, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa na Italia ambako pia aliwasilisha mpango huo huku akilenga pia kufanikisha azma ya Ukraine kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO.