1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Ufaransa: Migomo ya kupinga marekebisho ya umri wa kustaafu

7 Februari 2023

Migomo mipya ya kupinga marekebisho ya umri wa kustaafu nchini Ufaransa imeathiri usafiri wa umma na shughuli za shule, pamoja na umeme.

https://p.dw.com/p/4NCRJ
Frankreich I Anti-Corona Proteste in Paris
Picha: Alain Jocard/AFP/Getty Images

Vilevile shughuli za ugavi wa mafuta na gesi umeathirika nchini Ufaransa leo hii Jumanne kutokana na maandamano hayo yaliyohudhuriwa na maelfu ya watu wanopinga marekebisho ya serikali ya pensheni.

Duru ya tatu ya maandamano hayo imefanyika siku moja baada ya wabunge wa Ufaransa kuanza kujadili muswada huo wa pensheni ambao unalenga kuongeza umri wa chini wa kustaafu kutoka mika 62 hadi 64. Rais Emmanuel Macron anaunga muswada huo kuwa sheria katika muhula wake wa pili.