1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza kuipatia Ukraine mkopo wa dola bilioni 2.94

22 Oktoba 2024

Uingereza imesema itaipatia Ukraine mkopo wa dola bilioni 2.94 ili kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4m4ek
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer (kushoto) akiwa na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Waziri wa Ulinzi wa John Healey
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer (kushoto) akiwa na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Waziri wa Ulinzi wa John HealeyPicha: Richard Pohle/AP Photo/picture alliance

Fedha hizo ni sehemu ya mkopo uliopangwa kutolewa na Kundi la Mataifa Saba yaliyoinukia kiviwanda G7 na ambayo yanaiunga mkono Kiev.

Jumla ya fedha hizo ni kutoka kwenye mapato ya mali za Urusi yaliyozuiliwa na zitatumiwa kuisaidia Ukraine kununua silaha na kujenga upya miundombinu yake iliyoharibiwa na vita.

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza John Healey amesema pesa zitakazotolewa na Uingereza zitakuwa kwa ajili ya jeshi la Ukraine pekee na zitatumiwa kusaidia upatikanaji wa  droni zenye uwezo wa kusafiri mbali zaidi  kuliko baadhi ya makombora ya masafa marefu.

Hayo yakijiri, mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine usiku wa kuamkia leo yamesababisha vifo vya watu sita, watatu katika mji wa Zaporizhzhia na wengine katika mkoa wa Donetsk. Hayo yameelezwa na magavana wa maeneo hayo huku Urusi ikiendelea kukana kuwalenga raia.