1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza kuupigia kura muswada wa kupeleka wakimbizi Rwanda

19 Machi 2024

Mpango wa Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, wa kuwapeleka Rwanda waomba hifadhi nchini Uingereza ulikaribia kuwa sheria baada ya serikali kutupilia mbali mabadiliko yote yaliyopendekezwa na Baraza la Juu la Bunge.

https://p.dw.com/p/4dt3V
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, akiwa bungeniPicha: Jessica Taylor/UK Parliament/AFP

Mpango wa Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, wa kuwapeleka nchini Rwanda wahamiaji wanaotafuta hifadhi nchini Uingereza ulikaribia kuwa sheria hapo jana baada ya serikali kutupilia mbali mabadiliko yote yaliyopendekezwa na Baraza la Juu la Bunge.

Mswada huo ambao ulipingwa vikali na Mahakama za Uingereza zilizoamua kuwa Rwanda si nchi salama, utarejeshwa tena Bungeni siku ya Jumatano ili kupigiwa kura. Ikiwa utapitishwa bila kurekebishwa, basi unaweza kuwa sheria mapema wiki hii.

Waziri Mkuu wa Uingereza amesema ni muhimu kuufanikisha mpango huo wa kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda, kwa sababu nchi yake inahitaji kuweka vizuizi kwa wahamiaji wanaongia Uingereza kinyume cha sheria.