1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani haifanyi vya kutosha kudhibiti uhamiaji haramu

8 Desemba 2024

Utafiti wa maoni uliofanywa na shirika la YouGov umeonyesha kuwa asilimia 75 ya wajerumani wanaiona serikali haiko makini linapokuja suala la kudhibiti uhamiaji ulio kinyume cha sheria.

https://p.dw.com/p/4nt14
Deutsches Auswandererhaus, German Emigration Center
Deutsches Auswandererhaus, German Emigration CenterPicha: S. Ziese/blickwinkel/picture alliance

Uchunguzi huo uliowashirikisha wawakilishi 2,415 mwanzoni mwa mwezi huu pia umeonyesha kuwa asilimia 50 ya wajerumani wanaamini serikali haifanyi juhudi za kutosha za kuwawezesha wahamiaji wanaoweza kufanya kazi. 

Wanasiasa wataka sera kali zaidi za kuomba hifadhi na uhamiaji nchini Ujerumani

Asilimia 93 inauona uhamiaji haramu kama tatizo kubwa huku asilimia 2 ikiwa na maoni kwamba watu kutoka mataifa yalio nje ya Umoja wa Ulaya kuingia au kubakia Ujerumani bila vibali halali hakuleti tatizo lolote. 

Polisi ya shirikisho la Ujerumani, ilirekodi idadi ya watu 71,000 waliongia ujerumani bila vibali halali ndani ya miezi 10 iliyopita ikilinganishwa na 127,500 mwaka mzima wa 2023.