Ujerumani imeliondoa jeshi lake la mwisho Afghanistan
30 Juni 2021Katika taarifa yake waziri huyo mwenye dhamana ya ulinzi ametoa shukrani kwa askari wake kwa waume 150,000 ambao wamekuwa katika jukumu hilo tangu 2001, akisema wanajivunia utumishi wao.
Aidha amewakumbuka waliopoteza maisha katika operesheni hiyo, na wale ambao walijeruhiwa akisema hawatasahaulika maisha. Kwa mujibu wa jeshi la Ujerumani, wanajeshi 59 wameuwa tangu kuanza operesheni hizo.
Ujerumani ilikuwa na wanajeshi 1,100 nchini Afghanistan.
Kabla ya kuanza kujiondoa, Ujerumani ilikuwa na wanajeshi 1,100 ambao walikuwa wakihudumu kama sehemu ya wanajeshi madhubuti 9,600 wa Umoja wa Kujihami wa NATO ikiwa na nafasi ya pili kwa wingi baada ya Marekani. Wanajeshi hao walikuwa wakishiriki katika utoaji wa mafunzo na mipango mininge ya amani. Marekani imetangaza kujiondoa kabisa ifikapo Septemba.
Uingereza, Italia na Uturuki pia zina kiwango kikubwa cha wanajeshi nchini Afghanistan, ikielezwa mataifa mataifa matano yanafanya jumla ya wanajeshi 6,000. Lakini pia mataifa yaliokuwa na idadi ndogo katika operesheni hiyo ambayo ni Denmark, Estonia, Uhispania yamekwishawaondoa wanajeshi wao.
Hali bado ni ya mashaka katika maeneo mengi.
Hatua hii ya Ujerumani inatekelezwa baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kutangaza ameanza kuwandoa wanajeshi wake baada ya kuwepo kwa miaka 20. Aprili, wizara ya ulinzi ya Ujerumani ilitangaza mpango wa kujiondoa nchini Afghanistan hadi ifikapo mapema Julai.
Hatua hiyo inatekelezwa huku hali ya kiusalama nchini Afghanistan ikitajwa kuzorota siku hadi siku. Kundi la wapiganaji wa Taliban linatajwa kuchukua udhibiti wa zaidi ya wilaya 100 miongoni mwa wilaya zaidi ya 400 za taifa hilo. Na majeshi ya kigeni nchini Afghanistan yaliingia Oktoba 7, 2001, ikiwa si zaidi ya mwezi mmoja tangu mashambulizi ya 9/11 ambayo yalisababisha vifo vya takribani watu 3,000.
Chanzo: AFP