Ujerumani: Haijashirikiana na Israel huko Lebanon
14 Novemba 2024Vyanzo hivyo vya Hezbolllah vinasema wanajeshi hao wa Ujerumani wanoishirikiana na Israel wako nchini humo kama walinda usalama wa Umoja wa Mataifa.
Ujerumani kwa sasa inatoa wanajeshi 100 kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL, ambacho kimejipata katikati ya mapambano ya wanajeshi wa Israel na wanamgambo wa Hezbollah.
Israel yadai kuyashambulia maeneo zaidi ya 100 ya Hizbullah
Haya yanafanyika wakati ambapo watu kadhaa wameuwawa na wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel yaliyolenga majengo mawili ya makaazi katika Mji Mkuu wa Syria Damascus.
Jengo la kwanza lililolengwa lilikuwa mtaa wa Mazzeh na hilo la pili lilikuwa Qudsaya, magharibi mwa mji huo mkuu. Kituo cha redio cha jeshi la Israel kinasema mashambulizi hayo yalikuwa yanazilenga mali za kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Islamic Jihad.