1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuendelea kuisaidia Ukraine

20 Agosti 2024

Serikali ya Ujerumani imekanusha madai kuwa inapanga kupunguza msaada wake kwa Ukraine kutokana na hali ya uchumi kuwa ngumu.

https://p.dw.com/p/4jfYA
Ujerumani I Vita vya Ukraine na Urusi
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani asema ufinyu wa bajeti hautawazuia kuendelea mkuisaidia Ukraine kupambana na Urusi Picha: Christoph Reichwein/dpa-Pool/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema nchi yake haitabadili msimamo wake kwa Ukraine na amesisitiza kuwa misaada kwa ajili ya Ukraine itaendelea kwa muda mrefu kadri itakavyo hitajika.

Msemaji wa serikali Wolfgang Buechner alisema awali kwamba "kuripoti kwamba inasingizia kuwa tunapunguza misaada sio sahihi.

Ujerumani ni nchi ya pili kwa kutoa misaada mikubwa kwa Ukraine baada ya Marekani.