1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yamlaumu Guterres kukubali mwaliko wa Putin

22 Oktoba 2024

Ukraine imemtupia lawama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa kukubali mwaliko wa rais wa Urusi Vladimir wa kuhudhuria mkutano wa kilele wa BRICS utakaoanza Jumanne katika mji wa Kazan.

https://p.dw.com/p/4m4f9
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Picha: William Volcov/ZUMA Press Wire/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha ameandika kwenye ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa X kwamba Guterres alikataa mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa kilele wa amani uliokuwa ukijadili vita nchini Ukraine na uliofanyika Uswisi mwezi Juni, lakini amekubali mwaliko wa yule aliyemuita mhalifu wa kivita na kusema kuwa hilo ni chaguo baya linalotia doa haiba ya Umoja wa Mataifa.

Soma pia: Urusi kuwa mwenyeji wiki hii wa mkutano wa kilele wa BRICS

Wakati huo Guterres alieleza kuwa hatohudhuria mkutano huo lakini akasisitiza kuwa Umoja wa Mataifa uliwakilishwa. Rais wa Ukraine Volodoymyr Zelenskiy anatarajia kuandaa mkutano wa pili mwishoni mwa mwaka huu, lakini Urusi tayari imesema haina nia ya kuhudhuria.