1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yaomba misaada ziada ya kijeshi kuikabili Urusi

15 Aprili 2024

Ukraine imewaomba kwa mara nyengine tena washirika wake kuipa mifumo ya ulinzi, ili kuisaidia kujilinda dhidi ya mashambulizi ya angani kutoka Urusi yaliyolenga mifumo yake ya nishati katika wiki za hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4eoIZ
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ukraine Dmytro Kuleba
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ukraine Dmytro KulebaPicha: Efrem Lukatsky/AP/picture alliance

 

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ukraine Dmytro Kuleba aliuambia mkutano wa usalama kuhusu Ukraine kupitia vidio kwamba anachukua nafasi iliyopo kuwahimiza washirika wake wote kuchukua hatua za kijasiri na za kipekee kuipa nchi yake silaha.

 

Mashambulizi ya droni na makombora ya Urusi dhidi ya Ukraine, yamelenga miundombinu ya Kiev tangu mwezi Machi hatua iliyoifanya Ukraine kuongeza wito wake kwa washirika wake wa kupata usaidizi wa mifumo ya kujilinda.