SiasaUbelgiji
Ulaya yasema wameudhibiti uingiliaji kwenye uchaguzi
10 Juni 2024Matangazo
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Berlin leo Jumatatu, von der Leyen amesema wameona uingiliaji sio tu kutoka ndani ya Ulaya lakini pia kutoka nje, kuhusu maoni ya umma bila ya kutoa maelezo zaidi.
Von der Leyen ameonyesha kuridhishwa na matokeo ya vyama vya kihafidhina katika uchaguzi huo na kuongeza kuwa "Katika nyakati hizi za misukosuko, tunahitaji utulivu. Tunahitaji uwajibikaji na tunahitaji mwendelezo ambao nimeonyesha katika muhula wangu wa kwanza wa kile ambacho Ulaya yenye nguvu inaweza kufikia."
Haya yanajiri huku serikali ya Ujerumani ikipuuzilia mbali wito wa kufanyika uchaguzi wa mapema kutokana na matokeo mabaya ya vyama vya muungano unaounda serikali katika uchaguzi wa bunge la Ulaya.