Umoja wa Mataifa wataja "kushtushwa" na mauaji ya Kongo
9 Desemba 2022Matangazo
Tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini humo ilisema jana kuwa, mwezi uliopita, waasi wa M23 waliwaua takriban raia 131 wakiwemo wanaume 102, wanawake 17 na watoto 12 katika eneo la Mashariki mwa Kongo na kufanya vitendo vya ubakaji kwa zaidi ya watu 20.
Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekuwa na ukosefu wa utulivu kwa miaka kadhaa kutokana na kuwepo kwa makundi yenye silaha yakiwa ni urithi wa vita vya kikanda vilivyopamba moto mwishoni mwa karne iliyopita.
Kundi la M23, ambalo wengi wao ni Watutsi wa Kongo walianza tena mapigano mwishoni mwa 2021 baada ya kutosikika kwa miaka kadhaa.