SiasaAsia
Umoja wa Ulaya kuimarisha uhusiano na Ufilipino
31 Julai 2023Matangazo
Von der Leyen alitowa kauli hiyo baada ya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Ferdinand Marcus Jr. mjini Manila, ambapo wawili hao walijadiliana masuala kadhaa yakiwemo ya usalama, biashara na mabadiliko ya tabianchi.
"Usalama wa Ulaya na ule wa Bahari ya Hindi na Pasifiki havitenganishiwi. Umoja wa Ulaya umekuwa ukiunga mkono mazingira ya uhuru na ya wazi ya kanda hiyo, kwa sababu eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki lisilo na vitisho ni muhimu kwa uthabiti wetu, amani yetu na ustawi wa watu wetu." Alisema kiongozi huyo wa Umoja wa Ulaya.
Kwa miaka kadhaa sasa, Ufilipino imetumbukia kwenye uhasama na China kutokana kuwania udhibiti wa sehemu ya Bahari ya Kusini mwa China, ambayo Beijing inadai umiliki kamili.