Umoja wa Ulaya waanza mkutano wa kilele na mataifa ya Ghuba
16 Oktoba 2024Matangazo
Lengo la mkutano huo ni kukutana na mataifa sita tajiri ya Kiarabu yaliyopo kwenye baraza la ushirikiano la Ghuba ili kuwa na uhusiano wa kimkakati kwa kutambua ushawishi wa nchi hizo hasa katika migogoro kama vita vya Ukraine na huko Mashariki ya Kati.
Tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine,Umoja wa Ulaya wenye wanachama 27 umefanya mikutano kama hiyo na mashirika mengine ya kikanda ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama ya nchi za Kusini Mashariki mwa Asia-ASEAN pamoja na jumuiya ya CELAC inayoyakusanya mataifa ya Carrebean na Amerika Kusini.