SiasaUkraine
Makubaliano ya EU ya kuishtaki Urusi kwa uhalifu wa kivita
4 Machi 2023Matangazo
Von der Leyen amesema hatua ya kwanza muhimu itakuwa kuiwajibisha Urusi na Rais Vladimir Putin kwa uhalifu wa kutisha dhidi ya Ukraine na kufanya kila liwezekanalo ili kuwafikisha wahusika mahakani.
Rais huyo wa Tume ya Ulaya amebainisha pia kuwa kuna ushahidi unaoongezeka wa mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya raia, mateso na unyanyasaji wa kijinsia.
Soma pia:Putin 'sio mshukiwa pekee' katika uhalifu nchini Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema suala kuu ni kubaini jukumu la Urusi na viongozi wake kwa uchokozi na ugaidi dhidi ya Ukraine.