1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: China na washirika wake wanatumia wingi wao kulindana

11 Oktoba 2023

China na washirika wake wa kiimla wanatumia wingi wao kwenye Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kulindana dhidi ya uangalizi.

https://p.dw.com/p/4XOHL
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Human Rights Council katika mkutano wa Baraza na Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Human Rights Council katika mkutano wa Baraza na Haki za Binadamu la Umoja wa MataifaPicha: Benoit Doppagne/Belga/dpa/picture alliance

Matokeo ya hayo ni kwamba baraza hilo la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limegeuka kuwa chombo kinachoongozwa na nchi zilizo na rekodi mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu. 

Kulingana na kifungu cha kwanza 1 cha Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, "wanadamu wote wamezaliwa huru na sawa katika utu na haki."

Kazi ya Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa ni kufuatilia jinsi nchi zinavyoheshimu kanuni hii ya msingi, kuhakikisha kwamba watu wanaweza kuishi bila mateso na ubaguzi.

Nchi kadhaa zinazohudumu kama waangalizi wa haki za binadamu duniani, zina rekodi mbaya katika mataifa yao, huku China ikiongoza katika orodhahiyo, pamoja na Falme za Kiarabu na Eritrea.

Soma pia:Vladmir Putin, Xi Jinping na mikakati yao ya kutawala maisha

Katika miaka ya hivi karibuni kumerekodiwa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika mataifa hayo, kama vile uwepo wa kambi za mateso, kukamatwa kiholela, kazi ya kulazimishwa na kukandamiza upinzani.

Kadri idadi ya tawala za kimabavu zinavyoongezeka ulimwenguni, uwepo wao kwenye Baraza la Haki za Kibinadamu unaongezeka pia.

Hasa kwa China ambayo imetumia nafasi hii vibaya kwa kutegemea washirika wake kupiga kura au kujiepusha kupiga kura kwa kuzingatia masilahi yake ya kitaifa.

Mataifa yanao uhuru kamili katika kuamua?

Mnamo mwaka wa 2023, ni asilimia 30 tu ya nchi kwenye Baraza la Haki za Kibinadamu ziliainishwa kuwa "huru" kwa mujibu wa taasisi ya maoni ya Marekani ya Freedom House.

Katika ripoti yake ya kila mwaka yaUhuru Ulimwenguni, shirika hilo huchunguza iwapo serikali hufanya uchaguzi huru na kufikia viwango vya haki za kisiasa na uhuru wa kiraia, kama vile uhuru wa kukusanyika. 

Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa na mwenzake wa China Xi Jinping.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa na mwenzake wa China Xi JinpingPicha: Alexei Druzhinin/AP/picture alliance

Jumla ya asilimia 70 ya mataifa wanachama wa sasa wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa yaliorodheshwa kuwa "huru kwa kiasi fulani" kama vile India huku Sudan na mataifa mengine yakiorodhesha kuwa "sio huru."

Kila mwaka, Baraza la Haki za Kibinadamu huchagua theluthi moja ya wanachama wake 47 kwa mihula ya miaka mitatu kwa ukomo maalumu ya kijiografia inayozingatia idadi ya nchi za Umoja wa Mataifa kwa kila eneo.

Soma pia:Saudi Arabia inavyowafuatilia na kuwatisha wakosoaji walioko nje

Makundi ya Asia-Pacific na Afrika yana wanachama 13 kila moja, Ulaya Magharibi na Amerika Kaskazini zina wanachama saba, Ulaya Mashariki ikiwa na sita, na kundi la Amerika Kusini na Karibea lina wanachama wanane.

Uchaguzi wa muhula wa 2024 hadi 2026 unatarajiwa kufanyika mnamo Oktoba, wagombea ikiwa ni pamoja naCuba, Kuwait na Urusi, ambayo iliondolewa kwenye baraza hilo mnamo 2022 kufuatia uvamizi wake kamili nchini Ukraine.

Watafiti kutoka mashirika kama vile Freedom House, V-Dem na Demokracy Matrix wanajaribu kukadiria ufuasi wa wanachama kwa viwango vya kuheshimu haki za kibinadamu kimataifa kama vile uhakikisho wa uhuru wa raia na kufuata makatazo ya mateso.

Watawala wa kiimla wanazingatia maslahi yao

Kulingana na Yaqiu Wang, mtafiti mkuu wa China katika shirika la Human Rights Watch, moja ya athari za kuongezeka kwa tawala za kiimlani kwamba kura za Baraza la Haki za Kibinadamu mara nyingi zinalindana kwa kile alichokitaja kama "kuzingatia maslahi zaidi."

Kwa mfano Pakistan mara nyingi husimama na China katika kura, kwa sababu ya uhusiano wa kiuchumi, Pakistan inaiona China kama mshirika dhidi ya mpizani wake India. 

Mwanaharakati wa Iran Narges ashinda tuzo ya Nobel 2023

Licha ya madhumuni ya Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa, muundo wa sasa wa chombo hicho unakizuia kuwa na ufanisi katika vita dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Soma pia:Misri: Kura ya maoni kumruhusu el Sissi kutawala hadi 2030

Mara nyingi, nchi hizo ni washtakiwa na majaji katika kesi zao wenyewe za ukiukaji  na bila shaka hawana nia ya kujihukumu.

Ingawa wakosoaji wa baraza hilo wanakubali kwamba mabadiliko yanahitajika ili kurejesha chombo hicho katika malengo yake yaliyokusudiwa.

Wengi wamekuwa na mashaka kwa muda mrefu kuhusu mapendekezo maalum, kama vile kuweka kikomo uanachama kwa nchi ambazo zimebadilisha mikataba fulani ya haki za binadamu.