UN: Mshukiwa wa mauaji ya kimbari asifunguliwe mashtaka
8 Agosti 2023Majaji wa rufaa wa Umoja wa Mataifa wameamuru hapo jana kusitisha kesi ya mshukiwa wa mauaji ya kimbari Felicien Kabuga, wakisema ana matatizo ya akili, huku wakitupilia mbali pendekezo la kupunguza urasimu katika kesi hiyo.
Majaji hao ambao ni sehemu ya Mahakama ya uhalifu wa kivita ya Rwanda, wameamuru pia mahakama itathmini kwa haraka ni katika mazingira gani Kabuga mwenye umri wa miaka 80 anaweza kuachiliwa huru, jambo ambalo limekuwa likiombwa pia na wakili wake. Waendesha mashitaka wamekuwa wakidai kuwa kusitishwa kwa kesi hiyo, itakuwa sio haki kwa wahanga.
Mfanyabiashara huyo wa zamani aliyekuwa akimiliki kituo cha redio, alikuwa mmoja wa washukiwa wa mwisho waliokuwa wakisakwa na mahakama hiyo kwa mashtaka ya uhalifu wa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda. Kabuga alikamatwa nchini Ufaransa mwaka 2020 baada ya kusakwa kwa zaidi ya miaka 20.