UN: Nusu ya Wasudan wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula
28 Juni 2024Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNICEF, lile la chakula na kilimo FAO na la mpango wa chakula duniani WFP yamesema katika taarifa ya pamoja kuwa, nusu ya raia wa Sudan wanakabiliwa na changamoto ya kulisha familia zao.
Kwa mujibu wa ripoti iliyoandaliwa kwa kutumia kipimo cha kuboresha tathmini ya usalama wa upatikanaji wa chakula na mchakato wa kupitisha maamuzi, IPC, kuna hatari kubwa ya maeneo 14 nchini humo kukumbwa na baa la njaa iwapo vita kati ya jeshi na kundi la wanamgambo la RSF vitaaendelea.
Soma pia:Wataalamu wa UN watuhumu pande zinazopigana Sudan kutumia njaa kama silaha
IPC imeorodhesha maeneo ya mji mkuu Khartoum, Darfur, Kordofan na jimbo la El Gezira kama maeneo ambayo yanakabiliwa na changamoto ya uhakika wa kupata chakula.