1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaonya kuhusu vyombo vya majini kuharibu mazingira

29 Novemba 2022

UN yatahadharisha kuhusu vyombo vya majini kuharibu mazingira

https://p.dw.com/p/4KDZN
US Kohlekraftwerk Dave Johnson in Glenrock Wyoming
Picha: J. David Ake/AP Photo/icture alliance

Umoja huo umetowa mwito kwa sekta hiyo ya usafiri wa majini  kuzipiga marufuku meli zilizochakaa na zinazotowa moshi unaochafua mazingira pamoja na kuimarisha miundo mbinu ili kuharakisha kuingia kwenye mifumo isiyochafua mazingira. 

Shirika la Umoja wa mataifa la biashara na maendeleo,UNCTAD limetaja kuhusu dhima muhimu ya sekta hiyo ya usafiri wa majini katika uchumi wa dunia,ambapo zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa za bishara duniani husafirishwa kupitia baharini.  

Hata hivyo mkuu wa shirika hilo,Rebeca Grynspan amewaambia waandishi habari kabla ya kuzinduwa ripoti ya mwaka ya UNCTAD kuhusu usafiri wa majini,kwamba wakati dunia inafahamu umuhimu wa kupunguza gesi chafu ili kuzuia majanga ya mabadiliko ya tabia nchi, sekta hiyo imeshuhudia uzalishaji wa gesi chafu ukiongezeka kwa asilimia 4.7 kati ya mwaka 2020 na 2021 pekee.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW