1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yatoa wito kwa mataifa kuongeza juhudi kulinda mazingira

22 Januari 2025

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametilia mkazo onyo lake kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na kusema kiu ya dunia katika matumzi ya nishati ya visukuku ni hatua mbaya ambayo haitamuacha yeyote salama.

https://p.dw.com/p/4pTh5
UN-Sicherheitsrat |  UN-Generalsekretär Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitoa maelezo yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Picha: Richard Drew/dpa/AP/picture alliance

Pamoja na onyo hilo, lingine aliloligusua ni lile la kitisho kinachosababishwa na teknolojia ya Akili Mnemba yaani AI. Ratiba Guterres, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Jumatano hii imezongwa na msururu wa vikao na shughuli nyingi katika jukwaa hilo la kila mwaka la kiuchumi duniani.

Viongozi wa dunia kama mawaziri wakuu wa Uhispania na Malaysia, wasomina wasimamizi wa biashara walikuwa miongoni mwa wasomi wanaoshughulikia mada kadhaa kama vile kuhusu suala la uwezekano wa kukuza uchumi katika maeneo kama China na Urusi, na ahadi na hatari za Akili Mnemba, na huku lilikiwepo suala jipya kutoka Washington la kuanza kwa Muhula wa pili wa Rais Donald Trump ulioanza Jumatatu.

Rais Volodymyr Zelenskyy ahimiza msaada zaidi kwa taifa lake

Schweiz Davos 2025 | Ukrainischer Präsident Selenskyj spricht beim Weltwirtschaftsforum
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Kiuchumi la Dunia huko Davos, Uswizi, Jumanne, Januari 21, 2025.Picha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Rais Volodymyr Zelenskyy alishiriki katika kutoa mchango wake katika mikutano yake mbalimbali na hasa alipokutana na viongozi kama vile Rais wa Israel Isaac Herzog, Mwakilishi wa upinzani wa Ujerumani na Rais wa Vietnam Luong Cuong ikiwa kama sehemu ya jitihada zake za kuhamasisha uungwaji mkono kwa vita vya Ukraine dhidi ya Urusi.

Soma pia: Uharibifu wa kila kitu: Athari za kimazingira za mizozo

Akiwa na watendaji wa sekta ya nishati na teknolojia, Guterres alirejea katika mojawapo ya takwa lake la mara kwa mara akihimiza ulimwengu kufanya juhudi zaidi katika kupambana na ongezeko la joto duniani. Kadhalika alionesha masikitiko yake kwa namna mwaka wa 2024 ulivyokuwa wa joto zaidi kwenye rekodi, na alionya juu ya kupanda kwa kina cha bahariambacho kinaweza kutatiza shughuli za bandari zenye kusafirisha mafuta.

Zaidi Guterres anasema "Lakini linapokuja suala la vitisho vilivyopo, nyuklia haiko peke yake tena. Leo, tunakabiliwa na vitisho viwili vipya na vikubwa ambavyo vinahitaji umakini zaidi wa kimataifa na hatua kwa sababu vinatishia kuvuruga maisha kama tunavyofahamu. Mgogoro wa kimazingira na upanukaji usiodhibitiwa wa Akili Mnemba ambao unaweza kutumika kama nyenzo ya ulaghai."

Uharibifu wa mazingira ni mkubwa mijini

Kitisho cha hatua ya Rais Trump kuiondoa Marekani katika mkataba wa Paris

Katika mkutano tofauti na huo wa Guterres, Umoja wa Mataifa umesema hatua ya Donald Trump kuiondoa Marekani katika mkataba wa kimazingira ya Paris haipaswi kupunguza kasi ya ulimwengu kuelekea uwekezaji wa nishati mbadala ambayo mkataba huo ulianzisha. Celeste Saulo, ambae ni mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa amesema anaamini kuwa nchi nyingi zitaendelea kuelekea katika zingatio la nishati za kutunza mazungira.

Alipoingia madarakani rasmi siku ya Jumatatu, Rais Trump alitangaza kuiondoa Marekani katika mkataba wa Paris wa mwaka 2015 uliopitishwa na mataifa 195 katika kukabiliana na utoaji wa gesi chafuzi zinazosababisha athari za kimazingira.

Soma zaidi:Davos World Economica Forum

Wakosoaji wanaonya kuwa hatua hiyo inadhoofisha ushirikiano wa kimataifa katika kupunguza matumizi ya mafuta na inaweza kudhoofisha ahadi za nchi nyingine kwa hatua za kuyalinda mazingira.

Chanzo: AP/AFP