UN: Watoto 1,000 wanakufa kila siku kwa kunywa maji machafu
20 Machi 2023Matangazo
Taarifa iliyotolewa leo na UNICEF, imeeleza kuwa kila siku zaidi ya watoto 1,000 wenye chini ya umri wa miaka mitano wanakufa duniani kote kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu na mazingira machafu.
Soma pia:UNICEF: Mamilioni hawana maji safi Pembe ya Afrika
Kulingana na utafiti mpya wa UNICEF, jumla ya watoto milioni 190 kwenye nchi 10 za Afrika wako hatarini. Hali ni mbaya zaidi kwenye nchi za Benin, Burkina Faso, Cameroon, Chad, Ivory Coast, Guinea, Mali, Niger, Nigeria na Somalia.
Jumatano ni Siku ya Maji Duniani. Pia ni siku ya kuanza kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji.