1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi ni mwenyeji wa mkutano wa BRICS mjini Kazan

22 Oktoba 2024

Viongozi kadhaa wa dunia wanakusanyika nchini Urusi hii leo kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano wa kilele wa kundi la nchi zinazoinukia kiuchumi, (BRICS).

https://p.dw.com/p/4m53H
Urusi mwandazi wa mkutano wa BRICS Kazan
Urusi mwandazi wa mkutano wa BRICS wa siku mbili huko KazanPicha: Maxim Platonov/SNA/IMAGO

Mkutano huo wa kilele wa siku tatu katika mji wa Kazan ndio mkubwa zaidi wa aina hiyo kufanyika nchini Urusi tangu ilipoanza mashambulizi yake nchini Ukraine. Wakuu wa nchi 24 na serikali wanahudhuria mkutano huo na miongoni mwo ni Rais wa China Xi Jinping, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Masuala makuu katika ajenda ya mkutano huo ni pamoja na wazo la Putin la mfumo wa malipo unaoongozwa na BRICS kwa ajili ya kushindana na mfumo wa SWIFT, ambao ni mtandao wa kimataifa wa kifedha uliosimamisha benki za Urusi kuendesha kazi zake mnamo mwaka 2022. Mzozo unaozidi kuongezeka katika Mashariki ya Kati pia ni miongoni mwa maswala yatakayozungumziwa.