SiasaUrusi
Urusi yaanza mazoezi ya kijeshi katika ukanda wa Arctic
11 Aprili 2023Matangazo
Mazoezi hayo yanajumuisha wanajeshi karibu 1,800, manowari zipatozo 15 na ndege za kivita 40. Kulingana na kamandi hiyo, mazoezi hayo yana malengo ya kulinda usalama wa biashara za Urusi zinazopitia baharini pamoja na njia zake za majini, kama ujia wa kaskazini mashariki.
Mazoezi hayo yatahusisha pia majaribio ya mawasiliano kati ya vikosi vya angani, ardhini na vya majini.
Vikosi vya NATO, pia viliwahi kufanya mazoezi kama hayo katika ukanda wa Arctic, baada ya Urusi kuivamia kikamilifu Ukraine, mwaka uliopita.